Simon Mwangi March 25, 2023
2.3K views 0 Comments 2 Likes 0 Reviews
Raila Amollo Odinga, Mtoto wa Jaramogi Oginga Odinga. Kazaliwa tarehe 7 January 1945. Kweli Raila ni mchochole wa uongozi na ni wazi kwamba anatokana na ukoo wenye tamaa ya uongozi. Ni kweli kwamba hapo kale Imani yake ilikuwa thabiti. Odinga alikuwa mtetezi wa haki za Wakenya walalahoi na Kiongozi shupavu, mpaka tarehe 8 Agosti, 2017 alipowania kiti Cha uraisi na kupoteza kwa mpinzani wake Uhuru Kenyatta, aliyeshida kwa takriban kura 8,223,369. Chambilecho Wenye Ndimi Za Uhenga, Achanikaye Kwenye Mpini Hafi Njaa Vile Vile Mtaka Cha Mvunguni Sharti Ainame. Bwana huyu ni Mwehu , hakukubali kamwe kwamba kapoteza alizidi kung'ang'ania ushindi wake. Ndipo alipo kata kauli kuenda mahakamani akipinga ushindi wa Uhuru Kenyatta na William Ruto.
Baada ya Mahakama kusikiliza ushahidi uliotolewa walibananga kuwa uchaguzi haukuwa na uwazi. Mahakama yakaamuru uchaguzi wa uraisi kurundiwa baada ya siku 60. Zege huyu akawa na matumaini makubwa mno ya kushinda mara hii ya pili \ud83e\udd23\ud83e\udd23 lakini Bwege na wafuasi wake hawakushiriki uchaguzi. Tarehe 26, oktoba, 2017, uchaguzi wa uraisi ulifanyika na mambo yakatokea kinyume na matarajio yake na vibaraka wake. Uhuru Kenyatta na William Ruto walitangazwa washindi tena. Bwana Huyu ni Zege, Mwehu asiyejua kushindwa ni nini.
aah! Roho Kama ya babake Jaramogi Oginga Odinga. Baada ya Kenyatta kutangazwa mshidi, Odinga alipanga maandamano akikisia uchaguzi haukuwa halali, haya yalisababisha Vifo vya watu wengi, Uharibifu wa biashara,wizi, na uzorotaji wa uchumi wa Nchi. Tarehe 30 Januari, 2018, siku ambayo itasalia kumbukumbu kwa Wakenya wote ,siku iliyokuwa ya aina yake. Mzee anayefahamika na wengi Kama "Baba" Kicheche aliye na ushawishi mkubwa, Mzee Raila Odinga aliona vituko havitoshi akaamua kujiapisha Kama "peoples president" tukio hili lilitendeka katika bustani ya Uhuru park. Huyu Bwana akawa donda sugu kwa Raisi Kenyatta, Kenyatta akafahamu Ili uweze kulitatua jambo fulani ni vyema ukaangalia penye udhaifu ili usitumie nguvu kubwa, akakumbuka Raila ni Mhaini anayependa Uongozi zaidi ya chohote duniani. Kenyatta akamtafuta Raila, akamkaribisha chumbani na kuwa na mazungumzo naye walichosemezana Bado ni kitendawili kisichong'amuliwa na yeyote Kando ya wawili Hawa.
Baada ya kula gumzo Wawili Hawa walisalimiana mbele ya jopo la wanahabari na viongozi wachache kwa kishindo kikubwa na kukata kauli kufanya Kazi pamoja. Siku ya nyani kufa miti huteleza, Hiyo siku ikawa mwanzo wa masaibu ya Wakenya na viongozi wengine , Raisi na Naibu wake Wakawa Maji na mafuta , viongozi Kama Miguna Miguna akajua kweli Mla nawe Hafi nawe ila mzaliwa. Ukitaka kuruka Agana na nyonga. Kenyatta hakufanya maandalizi ya kutosha kabla ya kufanya uamuzi wa handshake. Jambo ambalo halikumpendeza Naibu Rais, William Ruto akaamua kuasi maamuzi ya Raisi kusalimiana na Odinga, pia wabunge wakatawanyika Kama kondoo wasio na mchungaji, Kuna wale waliomfuata Raisi wengine wakamfuata Naibu Raisi, Walio mfuata Naibu wa raisi walikiona Cha mtema Kuni, walilaumiwa, walikejeliwa wakadharirishwa lakini hawakutetereka wala kukata tamaa, ni hali ya kawaida.Ruto akafanyika kipenzi Cha wengi ,tabia zake za kumcha mungu, ukarimu na maneno ya kumtoa nyoka pangoni yakawa tiketi yake ya kuwania kiti cha uraisi Baada ya hatami ya Kenyatta.
Huyu Bwana Ruto akajua likiota liote na yakichacha yavumilie. Alizidi kuvumilia yote na kufahamu maisha ni safari, mtu hafai kukata kona. Hakuna marefu yasiyo na ncha: Tarehe 9,agosti,2022 siku iliyosubiriwa na wengi kwa hamu na hamumu, siku ya uchaguzi mkuu. Wakenya walijitokeza mkubwa kwa mdogo Ili kufanikisha haki zao za kidemokrasia . Kweli Mungu hamsahau mja wake. William Ruto na Imani yake, wanyonge, wakandamizwaji, na wanyonywaji waliamua kumpa madaraka kwa msimamo wake. Ruto akatangazwa kuwa raisi wa jamhuri ya Kenya na kuapishwa tarehe 13/9/2022.
Odinga ni Mwehu, ni kama mja laana, huyu bwana alilaaniwa Uongozi. Odinga mara nyingine akasema uchaguzi haukuwa na uwazi. Mzee mwenye heshima yake, Mzee anayestahili kutulia na familia yake, Huyo Kiguu na njia kaanza maandamano kusumbua serikali ya Ruto na kusababisha Vifo vya watu wengi, Uharibifu wa Mali ya umma,biashara,wizi, na uzorotaji wa uchumi. Raisi Ruto na Naibu wake Riggy G wamejitolea kwa nia, mvua na jua, panda shuka ,nenda rudi kuwanyia Wakenya Kazi. maandamano, vitisho na visasi vya wapinzani, vyote haviwashtui wala kuwarejesha nyuma. Tunataka kuona taifa hili likijikonboa kutokana na uchumi mbaya na wanyonge(hustlers) kujitawala.
Share this page with your family and friends.